Posts

Showing posts from June, 2022

Rami Tanzania mwenyeji Tuzo za (MAMA) MTV Africa Music Award 2023

Image
  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na makamu wa Rais na meneja mkuu wa Paramount Africa and Peer Lead BET International, Monde Twala,  na kukubaliana kushirikiana katika kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA- MTV Africa Music Award kwa mwaka 2023. Waziri Mchengerwa amekutana na Monde Twala Jijini Los Angeles   katika jimbo la California nchini Marekani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za BET kwa mwaka 2022. Katika mazungumzo hayo Waziri Mchengerwa amemwelezea nia na sababu ya Tanzania kutaka kuwa mwenyeji wa tamasha hilo la utoaji wa tuzo hizo kubwa za burudani kwa Afrika, kuwa ni kuongeza ushawishi kwa vijana wa kitanzania kuendelea kufanya vizuri katika sekta za burudani pamoja na kuitangaza zaidi Tanzania na uzuri wake katika ulimwengu. Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana  kuungana kwenye kutafuta washirika katika kuendesha tuzo hizo, na kuridhia kuwa maandalizi yaanze ma...

Ubingwa wa Yanga umeleta mshikamano- Mhe Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa kombe la katika ligi Kuu ya NBC katika msimu huu. Mhe. Mchengerwa  ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuchukua Ubingwa huo huku akipongeza mshikamano na furaha za mashabiki, ambazo wamezionyesha  wakati wa kukabidhiwa kombe hilo na mapokezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. " Kwa aina ya shangwe za ubingwa zilizofanyika jana na leo ni sawa na zile za mataifa yaliyoendelea ya Ulaya. Hakika mpira wa miguu ni mchezo mkubwa na pendwa duniani ambao huwaunganisha watu pamoja na kuleta amani, mshikamano, furaha na umoja baina ya wananchi" Ameongeza kuwa watanzania zaidi ya 90% ni wapenzi wa mchezo wa soka na amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inaboresha miundombinu ya michezo na kuleta usawa katika michezo hasa mpira wa miguu ili  kila mtanzania aweze kupata furaha.  "Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe...

Rais Samia aizindua MIF, aipongeza kwa kazi nzuri kwa watoto wa kike

Image
  Na John Mapepele Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan leo Juni 19, 2022 amezindua taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) iliyopo Zanzibar inayojishughulisha na kumkwamua mtoto wa kike katika elimu ili kutimiza ndoto zake yenye kauli  mbiu inayosema “lea mwana tung’are”. Kabla ya kuzindua taasisi hiyo, Mhe. Rais Samia ameupongeza uongozi wa MIF kwa mkakati kabambe wa taasisi hiyo wa kuleta chachu ya kuunganisha Serikali na MIF na taasisi nyingine katika kumkomboa mtoto wa kike kielimu huku akielekeza serikali inavyofanya maboresho izingatie masuala ya mitaala,ukaguzi wa elimu,utungaji wa mitihani na sifa za walimu.    Aidha, Mhe. Rais ametoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuunga mkono jitihada zinazofanywa na MIF huku akisisitiza kuwa suala la kuwakomboa Watoto wa kike ni suala la kila mtu. “Hilo ni jukumu letu sote, tunatakiwa wote tushirikiane.” Ameongeza Mhe. Rais Amezielekeza Wizara zinahusika na elimu kwa pande zote mbili ...
Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  kuwa Tanzania na India zinakwenda kupitia na kuboresha mikataba ya mashirikiano ya awali  kwenye eneo la Utamaduni na Sanaa iliyojiwekea  mwaka 1984 ili  kuiboresha iweze kuleta mapinduzi makubwa na ya haraka kwa faida ya pande zote. Mhe, Mchengerwa ameyasema haya leo Juni 17, 2022 akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Hassan Abbasi wakati alipotembelewa ofisini kwake na Balozi wa India nchini Mhe.  Binaya Srikanta Pradhan na kufanya mazungumzo ya kuendeleza mashirikiano kwenye sekta hizo. Aidha, amesema mambo mengi yalikubalika   baina ya nchi zote mbili hususan  kuendelea kwa tamaduni  pia  kumekuwa na mambo mengi ambayo yameandikwa ambayo kuna haja ya kufanya mapitio. Ameongeza  kuwa katika maongezi hao  wamekubaliana kuwa  na kituo maalum cha kuandaa filamu ambacho kitatumika kwa nchi za Afrika mashariki ambapo  baa...

Southampton kuwanoa makocha wa Tanzania- Mhe, Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  Tanzania inakwenda  kushirikiana na klabu ya Soka ya Southampton  kuwandaa makocha wa soka ili wawe kwenye kiwango cha kimataifa. Mhe. Mchengerwa amesema haya leo juni 17, 2022 ofisini kwake akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dk. Hassan Abbasi wakati alipokutana na ujumbe wa Klabu hiyo ulioongozwa na Afisa Biashara  Mkuu wa Klabu hiyo David Thomas.  Amesema dhamira ya Serikali ni kuona kuwa michezo mbalimbali inasimamiwa  kisayansi ili kuleta tija ikiwa ni pamoja na kuwa na makocha ambao watasaidia kufundisha  timu za micherzo ili kufuka kwenye kiwango cha kimataifa. Katika kikao hicho  wamekubalina kuwa Timu ya soka  ya ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls)  itakwenda kupatiwa mafunzo maalum   kwenye Klabu hiyo ikiwa ni maandalizi ya kwenda kwenye  mashindano ya kombe la dunia nchini India. Katika tukio hilo ...
Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Tanzania ya  Wanawake ya Kriketi kwa kufanya vizuri na kuongoza kwenye mashindano ya Kwibuka Cup yanayoendelea nchini hivi sasa nchini Rwanda. Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Juni 15, 2022 alipoongea na simu timu hiyo kupitia kwa Nahodha wa timu hiyo . Amesema anaipongeza timu hiyo  baada ya kuzishinda timu zote walizokutana nazo kwenye mashindano hayo na kuwa kinalani mwa mashindano hayo. Amezitaja timu hizo kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana na  Ujerumani  bado timu ya Nigeria na Brazil ambapo wakishinda mechi mojawapo wanaingia fainali za mashindano hayo. Aidha, amemshukuru Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe.  Meja Jenerali Richard Makanzo  kwa kuwa karibu na timu hiyo katika kipindi chote huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuisaidia timu hiyo ili ifike mbali zaidi.

Mhe. Mchengerwa awapongeza wadau kupaisha uchumi

Image
  Na John Mapepele   Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewapongeza wadau wa sekta za Sanaa na Burudani kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa taifa.   Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 imeeleza iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba imeeleza kuwa katika mwaka 2021 eneo la Sanaa na Burudani limechangia kwa asilimia 19.4 “Shughuli za kiuchumi zilikuwa na ukuaji mkubwa katika kipindi cha mwaka 2021 ni pamoja na Sanaa na Burudani (asilimia 19.4)” imefafanua sehemu ya taarifa hiyo. Katika kipindi cha mwaka 2020 eneo hilo lilichangia asilimia 13.7 hivyo kufanya ongezeko la asilimia 5.7 katika kipindi cha mwaka mmoja tu.  Wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa na burudani wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mikakati inayobuniwa na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ya kuinua na kuboresha sekta hizo katika kipindi kifupi. “Nimefarijika sana kusikia ...

TANZANIA NA MAREKANI ZAJADILI USHIRIKIANO SEKTA ZA SANAA NA MICHEZO

Image
  Na John Mapepele, Dar es Salaam  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa wakiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi wamekutana na Balozi wa Marekani hapa nchini leo Juni 8, 2022 wamekutana jijini Dar es salaam na kujadili masuala mbali mbali ya sekta za ikiwa ni pa moja na ujio wa msanii mashuhuri wa uchoraji ,Ashley Collins hapa nchini. Wakizungumza katika  kikao hicho ambacho Mhe. Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright ameambatana na Afisa Uhusiano wa Ubalozi huo, James Rodriguez wamejadili pia ujio wa Timu ya wachezaji nguli wanawake ya mchezo wa kikapu wa ligi  ya NBA nchini Marekani  hapa nchini ambao watakuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachezaji wanawake wa mchezo huo hapa nchini.  Waziri Mchengerwa amesema viongozi hao wamekubaliana  kuendeleza  malengo ya Royal Tour kwa kushirikiana zaidi  kwenye kuendeleza sekta  za sanaa na michezo ikiwemo kuendeleza...

TIMU ZA SERENGETI GIRLS NA TEMBO WARRIORS WAPEWA HESHIMA YA MASHUJAA TAIFA NA BUNGE

Image
  Na John Mapepele   Timu ya wanawake ya soka chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls) imeweka  historia  ya kuwa  timu ya  kwanza kupewa heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano kuingia  na kukaa kwenye viti vya mawaziri ndani ya bunge  baada ya kufuzu kuingia  mashindano ya dunia ikiwa ni heshima ya mashujaa wa Taifa kwa kazi kubwa iliyoifanya ambapo kesho ni zamu ya Timu ya soka ya Taifa ya Walemavu ya (Tembo Warriors) ambayo pia imefuzu  mashindano ya dunia ya soka kwa walemavu. Akiongea   mara baada ya kuketi eneo hilo rasmi la mawaziri, Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema ushindi huo unatokana  na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuiwezesha  timu hiyo katika kipindi chote cha  maandalizi wa  mashindano hayo. “Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha, kututia moyo na kutufuatilia kwa karibu sana katik...

Mhe. Mchengerwa atoa mambo 10 yanayoipaisha Tanzania duniani

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania imeandika historia ya kuingia kwenye mafanikio makubwa ya kidunia kwenye sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezio katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja chini ya Rais Samia suluhu Hassan. Akizungumza wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2022/23 ya Wizara yake bungeni leo,Juni 6, 2022.  Mhe, Mchengerwa amesema kutokana na ufanisi uliooneshwa na Tanzania katika maandalizi ya mashindano ya urembo, utanashati na mitindo kwa Viziwi ngazi ya Afrika, Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kidunia yatakayofanyik Oktoba, 2022 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.  Aidha amesema katika kipindi hiki Kiswahili kilipitishwa kuwa Lugha ya Kazi ya Umoja wa Afrika katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika tarehe 5 - 6 Februari, 2022 Jijini Addis Ababa, Ethiopia. Ameongeza kuwa Timu ya Taifa ya Soka la Walemavu (Tembo Warriors), i...

Mhe. Mchengerwa Ataja Makubwa ya Rais Samia katika Michezo, azindua mbio za CRDB Marathoni, Ajisajili kilomita 42

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekua mstari wa mbele siyo tu katika  kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika michezo  bali inashiriki moja kwa moja kuwekeza katika michezo kwa  kuwa inaamini kuwa michezo ni uchumi na biashara ambayo inatoa ajira nyingi kwa vijana. Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo Mei 5, 2022 kwenye uzinduzi wa msimu wa tatu wa mbio za kimataifa za CRDB kwenye viunga vya Nyerere jijini Dodoma ambapo amewataka wakuu wote wa mikoa na wilaya nchi nzima kuhamasisha michezo kwenye maeneo yao ili kusaidia wananchi kujenga afya, kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.  Aidha, amewaelekeza maafisa michezo na utamaduni katika kila mkoa na wilaya kuratibu mazoezi na mashindano ya michezo na sanaa ili kubaini na kuwatambua watanzania wenye vipaji kupitia program iliyoanzishwa na Serikali i...