Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia upya kanuni kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sanaa nchini Tanzania ili ziweze kuainisha bayana mfumo mzuri wa ufanyaji kazi unaowashirikisha wasanii binafsi, vyama, na mashirikisho ya Sanaa. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kupokea taarifa rasmi ya namna bora ya ya kusimamia HAKIMILIKI na Mirabaha kwa wasanii nchini kutoka kwa Kamati aliyoiteua Julai Mosi mwaka iliyoongozwa na Victor Tesha. “Mfumo huu utasaidia kuwatambua wasanii wote nchini na kuweza kuwahudumia kwa urahisi kwani mfumo uliopo sasa unatoa nafasi ya kila msanii kujitafutia riziki mwenyewe kitu kinachofanya wasanii wengi kukosa umoja na kuzalisha migogoro isiyokuwa na tija”. Amesisistiza Mhe, Mchengerwa Pia...
Popular posts from this blog
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Tanzania ya Wanawake ya Kriketi kwa kufanya vizuri na kuongoza kwenye mashindano ya Kwibuka Cup yanayoendelea nchini hivi sasa nchini Rwanda. Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Juni 15, 2022 alipoongea na simu timu hiyo kupitia kwa Nahodha wa timu hiyo . Amesema anaipongeza timu hiyo baada ya kuzishinda timu zote walizokutana nazo kwenye mashindano hayo na kuwa kinalani mwa mashindano hayo. Amezitaja timu hizo kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana na Ujerumani bado timu ya Nigeria na Brazil ambapo wakishinda mechi mojawapo wanaingia fainali za mashindano hayo. Aidha, amemshukuru Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo kwa kuwa karibu na timu hiyo katika kipindi chote huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuisaidia timu hiyo ili ifike mbali zaidi.
Maafisa Michezo simamieni vikundi vya mazoezi- Mchengerwa
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewaagiza maafisa michezo nchi nzima kuvisajili vikundi vyote vya mbio za hisani (Marathon) katika wilaya zao na kuvifuatilia ili kutoa motisha kwa vikundi vinavyofanya vizuri na kuwaandaa wanariadha kushiriki mashindano ya kimataifa na kusaidia kuzuia maradhi mbalimbali. Mhe, Mchengerwa ametoa agizo hilo leo, Aprili 10, 2022 wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mbio za hisani kwa ajili ya utoaji wa elimu na ufahamu kuhusu usonji zilizo andaliwa na taasisi ya Usonji ya Lukiza. Ameongeza kuwa wanariadha hao bora watakaopatikana kupitia mbio mbalimbali watashiriki mashindano ya kimataifa na kuliletea taifa medali mbalimbali. Akizungumzia mashindano ya Jumuiya ya madola, Waziri Mchengerwa amesema washiriki wote watakao kwenda kushiriki katika michezo hiyo Serikali inawahudumia, na wote wapo kambini wakiendelea kujiandaa vyema kuwakabili washindani wao katika m...
Comments
Post a Comment